Iran imerusha makombora zaidi ya 10 ikilenga Majengo ya Marekani yaliyopo Kaskazini mwa Iraq ikiwemo Kambi ya Jeshi ya Ain al-Asad ambapo kuna Majeshi ya Marekani ikiwa ni siku chache baada ya Marekani kumuua Qassem Soleimani.
Chaneli ya Taifa ya Iran imesema, Jeshi la Kimapinduzi la Nchi hiyo limevamia Uwanja wa Ndege wa Kambi ya Ain al-Asad na kutishia kufanya mashambulio zaidi iwapo Marekani itafanya mashambulio yoyote mapya.
Huku ikielezwa kuwa Iran imerusha makombora 13, katika taarifa yake imewaonya pia Washirika wa Marekani waliopo maeneo hayo kuwa nao pia Watashambuliwa iwapo watatumiwa na Marekani katika kuishambulia Iran.
Rais Trump pamoja na kusema atatoa taarifa leo, ila kupitia ukurasa wa Twitter amesema “Kila kitu kiko vizuri! Makombora yamerushwa kutoka Iran kwenda kwenye Kambi mbili za Jeshi zilizoko Iraq. Tathmini ya Majeruhi na uharibifu inafanyika sasa. Tuna vifaa vyenye nguvu na tumejidhatiti vizuri Kijeshi kuliko yeyote Duniani”.
MGANGA AMNYESHWA DAWA MWANAMKE YA KUMPUMBAZA NA MWANAMKE NA KUMBAKA