Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov ameonya hatari ya kutokea kwa vita vya tatu vya dunia huku akiitaja Nato kuwa ndio kiini cha suala hilo.
Katika mahojiano ya muda mrefu yaliyotangazwa na televisheni ya taifa ya Urusi , Lavrov alisema hatari ya mzozo wa nyuklia haipaswi kupuuzwa na kwamba msingi wa makubaliano yoyote ya kumaliza mzozo wa Urusi na Ukraine utategemea zaidi hali ya kijeshi baina ya mataifa hayo mawili.
Lavrov alishutumu vikosi vya Nato kwa kwa kusambaza silaha kwa wanajeshi wa Ukraine na kudai Urusi ilitaka kuzuia vita vya nyuklia kwa gharama yoyote. Akinukuliwa katika mahojiano na mashirika ya habari ya Urusi Waziri huyo alisema “Nato kimsingi inahusika katika vita na Urusi kupitia Ukraine na hivyo inampa Ukraine silaha jambo linaloweza kuzua hatari ya kutokea kwa vita vya dunia vya Nyuklia.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Urusi pia alikosoa mtazamo wa Kyiv katika mazungumzo ya amani na Moscow huku akisema “Kila Nia njema ina mipaka yake Lakini ikiwa hailingani, hiyo haisaidii mchakato wowote wa mazungumzo.”
Mahojiano hayo yalitangazwa saa chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin kutembelea Kyiv na kuahidi msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine.
Austin alisema Marekani ilitaka kuona Urusi inadhoofu na kuahidi kuipatia Ukraine silaha ili kuisaidia kushinda dhidi ya Moscow.
MWANZO MWISHO BASI LA WANA KWAYA NA LORI ZILIVYOGONGANA NJOMBE “DEREVA LA BASI KA-OVERTAKE”