Taasisi za Afrika Mashariki zinazohusiana na uhifadhi na kupambana na ujangili wamekutana jijini Dar es salaam kwaajili ya kupeana mbinu ili kutokomeza ujangili na kutunza mali ya asili.
Akizungumza na mwandishi Mkuu wa Idara za Operesheni za Kuzuia Ujangili kutoka taasisi ya Gulunet Fund, Fanikio Joseph alisema mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kupambana na ujangili katika kiwango cha kimataifa.
Alisema mwanzo walikuwa wakifanya makosa kwaajili ya kupambana na vita vya ujangili ndani ya nchi pekee, ambapo sasa hivi wanavuka mipaka kwa kuungana nchi mbalimbali ikiwemo nchi ya Kenya, Uganga na Congo Brazzaville.
Fanikio alisema nchi zote hizo zimeungana kwaajili ya kuunganisha nguvu za pamoja dhidi ya vita ya ujangili, kwakuwa nchi pekee yake haiwezi kudhibiti ujangili sababu ya mtandao kuwa mkubwa.
“Huu mtandao wa kijangili unatoka nchi moja kwenda nchi nyingine hadi kufikia nchi ambapo wao wanaona wanaweza kuzipata hizo Mali ghafi.
Kwahiyo mafunza haya ni mazuri kwakuwa yametujengea uwezo na inaturahisishia kiwa na ushirikiano katika vita dhidi ya ujangili” alisema.
Aliongezea kwa kusema taasisi ya Gulunet yenye makazi yake wilaya ya Serengeti kwa sasa imemilishwa vitalu viwili ambavyo ni Gulunet na Ikolongo.
Alisema vitalu hivyo wamekabidhiwa chini ya mamlaka Tanzania wild life pamoja na Serikali katika kusaidia Wanyama poli.
” Serikali zinapofanya kazi na taasisi hizi binafsi kunakuwa na ufanikisi Mkubwa zaidi, unaweza kukuta mwekezaji anaweka nguvu ya mtaji kwenye kupambana na ujangili wakati Serikali inawke miongozo ya kisheria na kitaratibu” alisema Fanikio.