Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.
Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.
Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid – The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.
Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.