Michezo

VIDEO: Arsenal imepata ushindi wa mechi 3 mfululizo kwa mara ya kwanza

on

Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu mwenendo na kiwango kibovu cha Arsenal katika mashindano mbalimbali wakiwa chini ya kocha wao mfaransa Arsene Wenger, mchezo wa nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Man City waliyopata ushindi wa magoli 2-1 umeonekana kuleta morali katika kikosi cha timu hiyo.

Arsenal usiku wa April 26 walikuwa wenyeji wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Leicester City katika uwanja wao wa Emirates kucheza mchezo wao wa 32 wa Ligi Kuu England msimu huu, Arsenal wao wanahangaika kumaliza katika TOP 4 ili wapate nafasi ya kucheza Champions League wakati Leicester wanajaribu kujinusuru na wimbi la kushuka daraja.

Katika game hiyo ambayo Arsenal alikuwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 baada ya Robert Huth wa Leicester kujifunga dakika ya 87 ya mchezo kutokana na kugongwa na shuti lililopigwa na Ignacio Monreal, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Arsenal kupata ushindi katika mechi tatu mfululizo za mashindano tofauti toka January 2017.

Kama utakuwa unakumbuka Arsenal alipata ushindi wa 2-1 wa FA dhidi ya Man City April 23, mchezo dhidi ya Middlesbrough wa 2-1 April 17 na leo amefanikiwa kupata ushindi wa 3 dhidi ya Leicester, Arsenal  sasa itarudi uwanjani Jumapili ya April 30 wakiwa ugenini kucheza dhidi ya Tottenham wakati Leicester City watakuwa ugenini April 29 kucheza dhidi ya West Bromwich Albion.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya mechi za April 26 2017.

VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF

Soma na hizi

Tupia Comments