AyoTV

VIDEO: Vodacom wameileta hii mpya msimu huu wa sikukuu

on

Leo December 13, 2016 Vodacom Tanzania imewaletea wateja wake promosheni mpya inayojulikana kama ‘Nogesha Upendo’ ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi ya fedha taslimu, muda wa bure wa maongezi na MB za Internet kila siku  katika msimu huu wa sikukuu.

Zawadi zenye thamani ya shilingi Bilioni 5 zitatolewa kwa wateja ambapo wateja wapatao  500 wataweza kujishindia shilingi milioni 1 kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo afisa mtendaji mkuu wa mawasiliano na uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia amesema……..

‘Promosheni hii itawezesha wateja wetu 500 kujishindia kila mmoja shilingi milioni 1/- katika droo za wiki na wengine watajishindia shilingi 100,000/- katika droo za kila siku katika msimu huu wa sikukuu kupitia promosheni hii’

‘Mbali na wateja kujishindia dakika tano za muda wa bure wa maongezi na kuperuzi internet, wateja wa Vodacom  pia kila watakaponunua vifurushi wataingizwa kwenye droo za kila siku na kila wiki za kujishindia vitita vya fedha, kiasi cha shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu katika msimu huu wote wa sikukuu’- Rosalynn Mworia

VIDEO: Unachotakiwa kukijua zaidi kutoka mtandao wa Vodacom, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments