Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliipongeza Marekani siku ya Jumatatu kwa “kuendelea uongozi na uungaji mkono” kwa nchi yake iliyokumbwa na vita wakati Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alipotembelea Kyiv.
“Yalikuwa mazungumzo yenye tija sana, na ni muhimu kwamba yalifanyika katika mkesha wa mkutano mpya katika muundo wa Ramstein,” Zelenskyy alisema katika taarifa kwenye tovuti ya rais.
Alisema ujumbe wa Austin pia ulijumuisha Jenerali wa Jeshi la Marekani Christopher Cavoli, Kamanda Mkuu wa Muungano wa NATO barani Ulaya.
“Tulijadili hali kwenye uwanja wa vita na matarajio yake – jinsi tunaweza kuimarisha ulinzi wetu na maendeleo yetu,” Zelenskyy alisema. “Kuna kifurushi kipya cha ulinzi kwa nchi yetu kutoka Merika.”
“Ninashukuru kwa hilo. Hasa, kutakuwa na silaha zaidi – makombora ambayo yanahitajika hivi sasa,” aliongeza.
Zelenskyy na Austin pia walijadili “vitendo vya Ukraine katika Bahari Nyeusi na ulinzi wa ukanda wetu wa usafirishaji,” taarifa