Michezo

Yanga wameimaliza Mwadui FC wanaisubiri Mtibwa Sugar mchezo wa kiporo

on

April 13 klabu ya Dar es Salaam Young Africans iliendelea na harakati zake za kumaliza viporo vya mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ilikuwa na viporo vitatu ila April 13 2016 imemaliza mchezo wake wa pili wa kiporo dhidi ya klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Yanga waliingia uwanjani wakiwa wanajua umuhimu wa mchezo dhidi ya Mwadui FC, kwani ilikuwa ni lazima wapate point tatu ili wajiweke katika nafasi nzuri, Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika ya 4 na Haruna Niyonzima dakika ya 87, wakati Mwadui FC waliambulia goli la kufutia machozi kupitia kwa Kelvin Sabato dakika ya 14.

DSC_0079

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha jumla ya point 56 wakiwa nyuma ya watani zao wa jadi Simba walio nafasi ya kwanza wakiwa na point 57 lakini wameizidi Yanga mchezo mmoja pekee. Yanga watashuka tena dimbani April 16 2016 kucheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments