Michezo

Mwadui FC washindwa kutamba katika uwanja wao wa Mwadui Complex dhidi ya Prisons

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo February 14 kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja vya Mkwakwani Tanga na uwanja wa Mwadui Complex, klabu ya Azam FC ilikuwa Tanga kumenyana na klabu ya Coastal Union ya Tanga, wakati Mwadui FC wakisalia katika dimba lao la nyumbani kumenyana na Tanzania Prisons.

DSC_0215

Mwadui FC ambaye dimba lake la Mwadui Complex linafahamika kama machinjio wameshindwa kutamba dhidi ya Tanzania Prisons na kuishia kuambulia suluhu ya 0-0. Kwa matokeo hayo Mwadui FC yupo nafasi ya 6, akiwa na point 29 na michezo 19.

DSC_0222

Wakati Tanzania Prisons wanakuwa nafasi ya tano kwakuwa na point 30 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 18. Kwa upande wa Tanga Azam FC wamekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Coastal Union ya Tanga.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments