Michezo

Kama yalikupita matokeo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara mtu wangu yapo hapa (+Pichaz)

on

Mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara ziliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, licha ya kuwa kuna mechi tatu ambazo zimeharishwa kutokana na wachezaji wake wengi kuitwa katika kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi, October 3 imepigwa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.

DSC_0145[1]

Mechi ambazo zimechezwa Jumamosi ya October 3 katika viwanja mbalimbali Tanzania ni mechi ya Maji Maji FC dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Maji Maji Songea, Mwadui FC ambayo inanolewa na kocha Jamhuri Kiwelu imeibuka na ushindia wa jumla ya goli 1-0 dhidi ya mwenyeji wake Maji Maji FC.

DSC_0146[1]

Joram Mgeveke akipiga krosi ambayo Marcel Bonveture akijaribu kuzuia

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kuona nyavu za mwenzake, dakika ya 56 kipindi cha pili Jabir Aziz akaiandikia goli Mwadui FC ya Jamhuri Kiwelu, goli ambalo lilidumu katika dakika zote tisini za mchezo na kuifanya Mwadui FC kuondoka na point tatu muhimu dhidi ya Maji Maji FC.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizopigwa October 3

  • Mgambo Shooting 0 – 0 Coastal Union 

DSC_0115[1]

Benchi la wachezaji wa akiba wa Mwadui FC Nizar Khalfan wa kwanza katika benchi

DSC_0124[1]

Mashabiki waliojitokeza kuutazama mchezo huo

DSC_0143[1]

Watu wa usalama walikuwepo pia mtu wangu

DSC_0153[1]

Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kiwelu akitoa maelekezo

DSC_0155[1]

Waamuzi wa mchezo

DSC_0159[1]

Benchi la Maji Maji FC wakiwa pamoja na kocha wao Mika Lonnstorm

DSC_0163[1]

Jerson Tegete na wachezaji wengine wakishangilia kwa pamoja goli la Jabir Aziz

DSC_0171[1]

Zote hizi ni mbwembwe za vijana wa Julio wakishangilia goli la Jabir Aziz

DSC_0179[1]

Jerson Tegete ambaye alikuwa nahodha wa mchezo baada ya kutolewa na kwenda benchi

DSC_0183[1]

DSC_0198[1]

Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kutazama mchezo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments