Michezo

Huku Ajib kule Bocco dakika 90 ya kuzitafuta point tatu kwa Azam FC na Simba, Cheki matokeo ya VPL Dec 12 (+Pichaz)

on

Baada ya mashabiki wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kukosa burudani hiyo kwa wiki kadhaa kutokana na kusimama kwa Ligi ili kupisha maandalizi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria na kupisha michuano ya Kombe la Challenge lililokuwa linafanyika Ethiopia na Uganda kuibuka mshindi wa taji hilo, December 12 Ligi imeandelea kama kawaida na michezo sita imepigwa.

DSC_0107

Ajib akidhibitiwa na Erasto Nyoni

Mchezo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ni mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Simba, huu ulikuwa ni mchezo ambao kwa upande wa Simba ulikuwa na presha kwa kocha wao mkuu Dylan Kerr ambaye kwa taarifa za chini ni kuwa uongozi ulikuwa hauridhishwi na mfumo wa ufundishaji wa kocha huyo.

DSC_0113

Hamisi Kiiza akijaribu kumtoka beki wa Azam FC Pascal Wawa

Mchezo ulianza kwa Azam FC kupata goli la kuongoza dakika ya kwanza ya mchezo baada ya John Bocco kutumia vizuri pasi ya Farid Mussa na kupata goli la uongozi, Simba walitulia na kufanikiwa kusawazisha goli dakika ya 24 kupitia kwa mshambuliaji wao Ibrahim Ajib na kwenda mapumziko wakiwa 1-1. Kipindi cha pili Simba walirudi kwa kasi na Ibrahim Ajib kumzidi ujanja beki wa Azam FC Said Morad na kupachika goli la pili dakika ya 68 ila John Bocco akasawazisha goli hilo na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa December 12

  • Stand United 0 – 2 Mwadui FC
  • Mgambo JKT 0 – 0 Young Africans
  • Kagera Sugar 1-1 Ndanda FC
  • Mbeya City 2-2 Mtibwa Sugar
DSC_0044

Himid Mao akijaribu kumdhibiti Mohamed Hussein wa Simba

DSC_0042

Mugiraneza akiwania mpira na Danny Lyanga

DSC_0066

Baada ya Simba kupata goli la kwanza Ajib na Hassan wakisali

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments