Michezo

Haya ni matokeo ya mechi ya Yanga Vs Tanzania Prisons (+Pichaz)

on

Kama kawaida  Jumatano ya September 16 kulikuwa na muendelezo wa mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti. Team ya millardayo.com inakupa nafasi ya kupata matokeo ya mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania bara inayomuhusisha Bingwa mtetezi.

DSC_0019

Deus Kaseke wa Yanga akidhibitiwa na James Josephat

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Dar Es Salaam Young African wamerudi nyumbani kucheza mechi yao ya pili, ikiwa ni muendelezo wa mechi zao za Ligi, Yanga ikiwa na wachezaji wake nyota na kikosi kilichosheheni wachezaji wake mahiri, kimeikaribisha timu ya Tanzania Prisons kutokea Mbeya katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

DSC_0005

Msuva akiugulia maumivu baada ya kuchezewa faulo

Yanga imeendeleza ubabe wake kwa kuifunga Tanzania Prisons kwa jumla ya goli 3-0 magoli ya Yanga yakifungwa na Mbuyu Twite, Amissi Tambwe na Donald Ngoma kwa mkwaju wa penati, huu ni ushindi wa pili kwa klabu ya Yanga baada ya mechi yake ya kwanza kucheza na kuifunga klabu ya Coastal Union ya Tanga kwa jumla ya goli 2-0.

DSC_0003

Msuva alipo jaribu kuonyesha utundu wake wa kuuchezea mpira

DSC_0022

Msuva akitafuta njia za kumpiga chenga James Josephat

DSC_0024

Mbuyu Twite akipiga shuti kali lililo ingia wavuni na kuifanya Yanga kupata goli la kwanza

DSC_0020

Donald Ngoma katika harakati za kutafuta nafasi za kufunga

DSC_0045

DSC_0060

Amissi Tambwe akipongezwa na wenzie baada ya kufunga goli la pili

DSC_0065

Mashabiki wa Yanga hawakuwa nyuma kushangilia

DSC_0089

Haruna Niyonzima akipiga faulo kuelekea lango la Prisons

DSC_0074

Mashabiki wa Prisons wakishangilia mwanzo hadi mwisho licha ya kupoteza mchezo.

DSC_0099

Golikipa wa Prisons akishindwa kudaka penati ya Ngoma

DSC_0112

Donald Ngoma akishangilia goli lake kwa staili ya kucheza muziki akiwa na Kaseke na Msuva

DSC_0117

Haji Mwinyi katika ubora wake wa kupiga krosi

DSC_0127

Amissi Tambwe akikwepa daluga

DSC_0132

Nurdin Chona akimdhibiti Geofrey Mwashiuya asichukue mpira

DSC_0141

Kocha wa Yanga akiongea na waamuzi wa mchezo baada ya mechi kumalizika

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments