Michezo

Full Time ya Yanga Vs Azam FC October 17 (+Pichaz)

on

October 17 ndio siku ambayo Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ulipigwa mchezo ambao uliamua nani atapata nafasi ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.

DSC_0024

Kikosi cha Yanga kilichoanza

Dar Es Salaam Young African walicheza dhidi ya Azam FC, mechi hii ilikuwa ni moja kati ya mechi za kuvutia, kwani Yanga na Azam FC zote zina point  15 kila mmoja na wote wamecheza jumla ya mechi 5 ila hii ilikuwa ni mechi ya sita kwa timu zote mbili. Kabla ya mechi kumalizika Yanga alikuwa anaongoza msimamo wa Ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, lakini mechi imemalizika kwa sare ya goli 1-1.

DSC_0030

Kikosi cha Azam FC kilichoanza

Kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika dakika ya 45 Donald Ngoma alipachika goli la kwanza baada ya kuitumia pasi safi kutoka kwa Juma Abdul, kipindi cha pili Azam FC walifanya mabadiliko kwa kumtoa Alan Wanga na kumuingiza Kipre Tchetche mshambuliaji ambaye alitumia vizuri pasi ya Farid Musa dakika ya 83 na kusawazisha goli. Licha ya Yanga kupata penati walishindwa kuitumia baada ya Kamusoko kupeleka mikononi mwa Aishi Manula,

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu October 17

  • Maji Maji 1 – 0 African Sports
  • Mbeya City 0 – 1 Simba
  • Ndanda FC 0 – 0 Toto African
  • Stand United 3  – 0 Tanzania Prisons
  • Coastal Union 0 – 1 Mtibwa Sugar
DSC_0064

Alan Wanga akijaribu kumtoka Haji Mwinyi wa Yanga

DSC_0074

Mbuyu Twite wa Yanga akidhibitiwa na Agrey Morris

DSC_0058

Alan Wanga akidhibitiwa na Nadir Haroub

DSC_0056

Kocha msaidizi wa Azam FC Mario Marinca akimpa maelekezo John Bocco

DSC_0080

Shomari Kapombe na Haji Mwinyi wakiwania mpira

DSC_0082

Mbuyu Twite akimdhibiti Himid Mao asipite kuelekea langoni kwao

 

 

DSC_0100

Mashabiki wa Yanga baada ya timu yao kupata goli la kuongoza

DSC_0128

Msuva na Juma Abdul wakijaribu kumkaba kwa pamoja Farid Musa

DSC_0144

John Bocco akiwa katika harakati za kutafuta goli la kusawazisha

DSC_0167

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli la Tchetche baada ya kusawazisha.

DSC_0163

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli la Tchetche baada ya kusawazisha.

DSC_0175

Simon Msuva akipatiwa matibabu baada ya kufanyiwa faulo ndani ya uwanja

IMG_0845

Donald Ngoma akishangilia baada ya kufunga goli

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments