Michezo

Haya ni matokeo ya mechi zingine za Ligi Kuu Tanzania Bara September 16

on

Matokeo ya mechi zingine za Ligi Kuu Tanzania bara kama yamekupita mtu wangu ninayo hapa, klabu ya Mgambo JKT  imepokea kipigo cha goli 2-0 toka kwa klabu ya Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani Tanga. Klabu ya Mbeya City imeifunga klabu ya JKT Ruvu goli 3-0 mechi imepigwa uwanja wa Sokoine Mbeya.

Stand United ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Kambarage Shinyanga, licha ya kupata udhamini mnono kutoka kwa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji madini, imekubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa Azam FC, magoli yakifungwa na Alan Wanga na Frank Domayo.

Toto African inayofundishwa na mzee John Tegete baba mzazi wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga Jerson Tegete imekubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara imeichapa klabu ya Coastal Union ya Tanga kwa goli 1-0 mechi ilichezwa katika uwanja wa nyumbani wa klabu ya Ndanda FC Nangwanda Sijaona Mtwara. Mwadui FC iliyochini ya koch Jamhuri Kiwelu imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya African Sports ya Tanga, ikiwa imepoteza mechi yake ya pili mfululizo toka Ligi Kuu Tanzania bara ianze

MATOKEO MECHI ZINGINE ZA LIGI KUU TANZANIA BARA September 16
Mgambo JKT 0-2 Simba SC
Mbeya City 3-0 JKT Ruvu
Stand United 0-2 Azam FC
Toto Africans 1-2 Mtibwa Sugar
Ndanda FC 1-0 Coastal Union
Mwadui FC 2-0 African Sports

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments