AyoTV

VIDEO: Rammy na furaha ya dili 3 Nigeria.. Mapenzi motomoto kwa Masogange

on

Staa kutoka Bongo Movie Rammy Galis alfajiri ya April 27 2016 alirudi Dar es Salaam akitokea Nigeria alipokwenda kufanya filamu aliyoshirikishwa na director wa Nigeria ambapo baada ya kurudi akiwa Airport Dar es salaam alithibitisha kupata dili nyingine mbili za kufanya movie Nigeria hivyo jumla ni tatu.

Nimerudi na zawadi kubwa sana kwa watanzania kwa maana Nollywood imenipokea vizuri, nilienda kwa ajili ya filamu moja lakini nimefanikiwa kufanya nyingine mbili, kutambulishwa huko ni kitu kikubwa nafikiri hata baada ya marehemu Kanumba kufariki hakukuwa na msanii zaidi yake aliyefanikiwa kwenda huko lakini nimepata bahati>>> Rammy Galis

Pamoja na hayo ya Nigeria, Rammy Galis na Masogange sasa hivi sio siri tena baada ya kuonekana kwenye mapozi ambayo tukijumlisha na ile Interview iliyopita AyoTV ni wazi kwamba wawili hawa wako kwenye uhusiano wa kimapenzi, tazama hii video hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Couple mpya town? Masogange na Rammy Galis

Soma na hizi

Tupia Comments