Habari za Mastaa

FORBES LIST: Mastaa 10 wanaolipwa pesa nyingi kupitia akaunti za Youtube 2016

on

Jarida linalofatilia maisha na shughuli za mastaa wakubwa duniani la Forbes limetoa orodha ya watu 10 ambao wanaingiza pesa nyingi kupitia akaunti zao za YouTube kwa mwaka 2016. Na mwaka huu mastaa hao wameingiza zaidi ya dola milioni 70.5 za Marekani huku star aliyelipwa zaidi akiwa na dola Milioni 15.

Nimekuwekea hapa full list ya mastaa 10 walioingiza pesa nyingi zaidi kupitia YouTube 2016.

1. PewDiePie (Felix Arvid Ulf Kjellberg) –  Dola Milioni 15 = (Tsh. Bilioni 33,216,750,000.00)
2. Roman Atwood  – Dola Milini 8 = (Tsh. Bilioni 17,715,600,000.00)
3. Lily Singh  – Dola Milioni 7.5 = (Tsh. Bilioni 16,608,375,000.00)

4.SMOSH (Ian Andrew Hecox na Daniel Anthony Padilla) – Dola Milioni 7 = (Tsh. Bilioni 15,501,150,000.00)
5. Tyler Oakley – Dola Milioni 6 = (Tsh. Bilioni 13,286,700,000.00)
6. Nerdy Nummies – Dola Milioni 6 = (Tsh. Bilioni 13,286,700,000.00)
7. Mark Fischbach (Markiplier) – Dola Milioni 5.5 = (Tsh. Bilioni 12,179,475,000.00)
8. German Garmendia – Dola Milioni 5.5 = (Tsh. Bilioni 12,179,475,000.00)
9. Miranda Sings (Colleen Ballinger) – Dola Milioni 5 = (Tsh. Bilioni 11,072,250,000.00)
10.  Good Mythical Morning ( Rhett McLaughlin, Charles ‘Link’ Neal III) – Dola Milioni 5 = (Tsh. Bilioni 11,072,250,000.00)

Forbes imetaja idadi ya watu waliojisajili na kuzifatilia akaunti za mastaa hao kama ifuatavyo.

1. PewDiePie — Watu wanaomfuata: Milioni 49,756,391

  • Mmiliki wa akaunti hii aliacha masomo ya chuo kikuu na kuamua kuanzisha akaunti ya YouTube ambayo ni ya kwanza duniani kufikisha views bilioni 10 huku akiongoza list hii kwa miaka miwili mfululizo.

2. Roman Atwood — Watu wanaomfuata: Milioni 10,152,692 

  • Akaunti hii inamilikiwa na staa ambaye amekuwa akiweka video za kuwatisha au kuwashtua watu kwa matukio ya kushangaza au kutotarajiwa na anapewa udhamini mkubwa kupitia kampuni ya karatasi za chooni ya Scott Toilet Paper.

3. Lily Singh — Watu wanaomfuata: Milioni 10,296,350

  • Huyu ni mchekeshaji ambaye anatumia akaunti yake ya YouTube kuingiza pesa ambapo mpaka sasa amefikisha views bilioni 1.3 ya kazi anazozipost.

4. SMOSH — Watu wanaomfuata: Milioni 22,474,510

  • Ian Andrew Hecox na Daniel Anthony Padilla, wote wakiwa na umri wa miaka 29 wanaunda kundi uchekeshaji la SMOSH wakiwa ni marafiki tangu wakiwa watoto wadogo.

5. Tyler Oakley — Watu wanaomfuata: Milioni 8,087,829

  • Tyler Oakley anaingia kwa mara ya kwanza kwenye Forbes list, na udhamini anaoupata kwa kurusha show za TV za Ellen DeGeneres umemfanya kuingiza pesa ndefu kwa mwaka huu. Matangazo ya midoli ya watoto ya Kellie Pickler, mahojiano aliyofanya na Hillary Clinton pamoja na Michelle Obama pamoja na ushirika wake na kampuni ya sheria ya LGBT youth zimekuwa chanzo kikubwa cha fedha alizoingiza mwaka huu.

6. Rosanna Pansino — Watu wanaomfuata: Milioni 7,398,450

  • Huyu ni mtangazaji wa kipindi cha mapishi cha Nerdy Nummies, ingawa yeye anakiita Geeky Cooking Show. Akaunti yake imekuwa ikiingiza pesa nyingi kutokana na aina ya kipekee ya style za mapishi yanayooneshwa ambapo mpaka sasa ameshapandisha zaidi ya video 100 zilizoifanya akaunti hii kutajwa na jarida la New York Times’ kama akaunti inayouza zaidi.

7. Markiplier — Watu wanaomfuata: Milioni 15,523,276

  • Mark aliamua kuacha masomo ya chuo kikuu na kuanzisha akaunti hii ili kutumia kipaji chake cha kuongea na kutoa ushauri kwa watazamaji ambapo imemfanya kuwa kati ya mastaa wanaolipwa pesa nyingi duniani kupitia YouTube.

8. German Garmendia — Watu wanaomfuata: Milioni 30,317,411

  • Hii inatajwa kuwa ndiyo akaunti ya yenye wafuasi wengi zaidi inayotumia lugha ya Kihispania ikiwa na wafuasi zaidi ya Milioni 30. Pia kuna video za bendi yake ya Ancud. Garmendia anakuwa staa mdogo zaidi chini ya miaka 26 kuwemo kwenye list ya Forbes.

9. Colleen Ballinger — Watu wanaomfuata: Milioni 7,359,094

  • Colleen Ballinger ni muimbaji ambaye hana uwezo kusikia lakini hiyo haijamfanya kuwa tegemezi, anamiliki akaunti inayomuingizia pesa nyingi kutokana na video zake anazopost akiimba, pia aliwahi kuwa muigizaji wa vipindi vya TV vya Off-Broadway na aliwahi kuongoza show ya The View pamoja na kutoa kitabu kilichouza zaidi cha Self-Help.

10. Rhett and Link — Watu wanaomfuata: Milioni 11,545,537

  • Rhett James McLaughlin na Charles Lincoln ‘Link’ Neal III wanafahamika kwa video zao za vichekesho Rhett and Link na wote wawili ni mainjinia waliosoma chuo kikuu cha North Carolina State ambao walifanya kazi kwenye makampuni makubwa lakini waliamua kaucha kazi na kufanya kazi ya uchekeshaji. 

VIDEO: Unafahamu kwamba kuna watu wananunua Views YouTube? Ommy Dimpoz ameeleza hapa kinachofanyika, Bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments