Mamia ya wananchi wa kata ya murieti mtaa wa kimara mwisho katika jiji la Arusha wameandamana kwa kufunga barabara
zaidi ya saa 6 huku wakiwatumbukiza kwenye madimbwi ya maji machafu diwani wa kata ya Murieti Francis Mbise na mwenyekiti wa mtaa nakuwatembeza kwenye maji hayo
Kwa madai ya kushindwa kuwasaidia kwenye barabara hizo kwa kipindi cha miaka 5 huku wakiomba serikali kuwasaidia
Mama chudaa Ambaye ni mwananchi wa eneo hilo akizungumza baada ya kufunga barabara hiyo amesema kuwa viongozi wamekuwa wakipita wakiwa na magari lakini wao wanateseka ile hali kuna mlima unaochimba mchanga nakuuzwa lakini wao wameshindwa kusaidiwa
“Sisi tumewaambiwa polisi watupige mabomu watuvunje mguu lakini sisi tunaamani hatufanyi vurugu,mimi nilianguka katikati ya maji nikaumia kichwani”Chudaa