Top Stories

Vurugu zazuka mkutano wa Ruto

on

Vurugu kubwa zilizuka jana kwenye viwanja vya Jacaranda jijini Nairobi kwenye Mkutano wa kisiasa uliokuwa ukiongozwa na Naibu Rais wa Kenya William Ruto.

Ruto ni mmoja ya Wagombea Wakuu wa Urais kwenye Uchaguzi ujao utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Vurumai hiyo ilisababishwa na vijana wanaompinga Naibu Rais kuvamia Mkutano huo.

Polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya vijana hao waliovia Mkutano huo.

Hata hivyo vurugu hizo hazikumzuia Mgombea huyo kuendelea na Mkutano wake huku akisaka kura na kuuza sera za Chama chake cha UDA.

Soma na hizi

Tupia Comments