Hatima ya vurugu zilizotokea katika mgodi wa kitalu C unaomilikiwa na Serikali na mwekezaji mzawa Onesmo Mbise pamoja na kitalu B unaomilikiwa na Saitot Mollel itajulikana March 24 mwaka huu baada ya timu ya wataalamu kutoka Dodoma na maofisa wengine kuingia ndani ya migodi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake,Afisa Mfawidhi wa Madini Mkoa wa Manyara, Mernad Msengi alisema kuwa timu ya Wataalamu wa ramani migodi imeshafika na imeshaanza kazi toka march 20 mwaka huu na ndani siku zisizozidi sita taarifa rasmi ya madini ya Kilo 4 itakuwa tayari kama madini hayo ni ya kitalu C au la.
Msengi alisema timu hiyo ya Wataalamu inafanya kazi kwa muda wote ndani ya mgodi kushirikiana na vyombo vyote vya dola katika Wilaya ya Simanjiro{Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Simanjiro}, Viongozi wa Mgodi wa Kitalu C na B na baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Madini lengo ni kutaka taarifa za kiuchunguzi ziwe wazi na zisiwe na kificho ili kuondoa lawama zisizo za Msingi kwa pande zote.