Top Stories

Vuta ni kuvute ACT Wazalendo, Membe asema yeye ndie Mgombea Urais

on

Bernard Membe amekanusha taarifa za kuwa wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika ngazi ya Urais akiseme yeye ndio Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo.

Membe amesema, “Mimi ndiyo Mgombea Urais wa JMT kupitia Chama cha ACT-Wazalendo. Mimi ndiye niliyekabidhiwa Ilani ya Chama hicho kuinadi kote nchini kwenye Uchaguzi huu”.

Kauli yake inakuja baada ya Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad kumuidhinisha Tundu Lissu (CHADEMA) kuwa Mgombea wao wa Urais wa Tanzania.

LIVE: MGOMBEA WA URAIS CCM, DKT. MAGUFULI AKIENDELEA NA KAMPENI

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments