fB insta twitter

‘Sasa UKIMWI kupimwa nyumba kwa nyumba’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.

Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la JamboLEO yenye kichwa cha habari ‘Sasa UKIMWI kupimwa nyumba kwa nyumba”

Gazeti la JamboLEO limeripoti kuwa Serikali inakusudia kufanya utafiti kwa kupima virusi vya UKIMWI (VVU) nyumba kwa nyumba kuanzia ngazi ya kaya, ili kupata takwimu sahihi kuhusu hali ya maambukizi mapya ya ugojwa huo ulivyo sasa nchini.

Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa ambapo alisema utafiti huo utakaotumia teknolojia ya kisasa, unalenga kupima viashiria na matokeo ya UKIMWI nchini, ili kujua ni kiwango gani Tanzania imepiga hatua katika kupamban na ugonjwa huo.

Gazeti hilo limemnukuu Dk Albina Chuwa akisema ……>>>”utafiti huo utafanyika kwa kutumia sampuli wakilishi ya kaya takribani 15, 800 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa kufikia walengwa 40, 000 wakiwamo watoto wasiopungua 8, 000′.

ULIKOSA KUTAZAMA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNI 24 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments