AyoTV

VIDEO: Isikupite hii Bajeti ya Wizara ya Viwanda zaidi ya bilioni 81 ilivyowasilishwa bungeni

on

Mei 6 2016 Waziri wa Viwanda, biashara na Uwekezaji Charles Mwijage aliwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017.

Katika hotuba yake, Waziri Mwijage aligusia sekta mbalimbali kama vile Viwanda vidogo na Biashara ndogo, Masoko. ..>>>’Ujenzi wa uchumi wa viwanda ni vita, tena vita kubwa sana. Mafanikio katika uchumi wa viwanda yatasababisha nchi yetu kuwa Taifa la watu wa kipato cha kati

Katika mwaka 2016/2017, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya Shilingi Milioni 20 ikilinganishwa na lengo la Shilingi Milioni 12 na elfu 14 kwa mwaka 2015/2016 kutokana na ada za leseni, uuzaji wa nyaraka za zabuni, faini kwa kukiuka Sheria ya leseni na makusanyo mengineyo

Katika mwaka 2016/2017, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inaomba kutengewa jumla ya Shilingi 81,871,992,000, ili kutekeleza majukumu ya Wizara.  Ni jukumu kubwa na nyeti ambalo linapaswa kuendelea kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote hasa Watanzania wazalendo

Unaweza kuendelea Kumsikiliza hapa chini kwenye hii video….

ULIIKOSA KUCHEKA KIDOGO NA HII YA LEO KUTOKA BUNGENI?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments