Top Stories

Siku 7 baada ya kushikiliwa, Dereva wa Dongote kafika Mahakamani

on

Dereva wa Kampuni ya Dangote Cement inayomilikiwa na Mfanyabiashara tajiri Afrika, Aliko Dangote, Khalid Sadik (39) na wenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Kisutu leo September 27, 2017 wakikabiliwa na kosa la kusafirisha raia wanane wa Ethiopia waliokuwa wanakwenda Afrika Kusini.

Mbali ya Sadik washtakiwa wengine ni Hussein Hassan (konda) na Juma Mtambo (Sonara) ambao wote ni raia wa Tanzania.

Aidha, washtakiwa wengine ambao ni Raia wa Ethiopia, ni Solomon Ertiso, Gezahegu Tiroro, Haile Latso, Thadeus Lilanso, Dawit Kuruse, Deznet Godebo, Feraru Hadago na Elioj Akola.

Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 5 akisema kuwa raia wa Ethiopia wanakabiliwa na kosa la kuingia nchini kinyume na sheria ambapo wanadaiwa September 20, 2017 walikutwa maeneo ya Mbagala Kongowe kinyume na sheria.

Aidha, wanadaiwa, September 20, 2017 waliingia nchini na kukutwa maeneo ya Mbagala Kongowe wakiishi bila kuwa na Viza.

Katika kosa jingine la usafirishaji wa magendo, linalowalabili Watanzania, inadaiwa September 20, 2017 maeneo ya Mbagala Kongowe na Mtoni Mtongani walikutwa wakisafarisha watu kimagendo na inadaiwa katika tarehe hiyo, walikutwa wakiwasafirisha binadamu kwa kutumia semi trailer ambalo ni mali ya Dangote Cement kuelekea Afrika Kusini.

Baada ya kusomewa makosa hayo, raia wa Ethiopia walikiri kosa na raia wa Tanzania walikana ambapo Wakili Mlay alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Nongwa amesema washtakiwa waliokana makosa wanaweza kupata dhamana kwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu huku washtakiwa waliokiri kosa wanatakiwa kusomewa maelezo ya awali ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi October 10 na 11, 2017.

Mkurugenzi alivyoacha Ofisi na kuingia chini ya Daraja kuzoa taka

Soma na hizi

Tupia Comments