Top Stories

Vyombo vinne vya habari vimekutana, Kusaga apongeza hili

on

Kutoka Serena Hotel Dar es salaam leo limefanyika tukio la kipekee lililovikutanisha vyombo vinne vya habari hapa nchini ambavyo ni TBC, Clouds Media Group, Mwananchi Communication Limited na Wasafi Media ambao wameungana kupitia kampeni rasmi ya Kuadhimisha Miaka 60 ya Uhuru iliyo pewa Jina la 60 Pamoja.

Miongoni mwa waliohudhuria ni CEO wa CMG, Joseph Kusaga ambaye amesema “Ni ukweli usiopingika kwamba vijana wengi wa sasa hawajui mambo mengi ambayo Taifa hili limewafanyia lakini ukweli Taifa hili limewafanyia mambo mengi sana ya kujifunza”

“Niwashukuru sana TBC kwa speed ambayo mnayo, nyinyi mmekua mfano wa sisi, mmetuongoza, mmetengeneza barabara miaka mingi wengine tumekuja kuirekebisha kidogo lakini nyie lazima tuwape makofi mengi sana TBC”

“Leo ni kama Sherehe na ni historia kuhakikisha vyombo vikubwa kama hivi vinaungana na kuwa kitu kimoja, nawapongeza kamati nzima, hawajala, kama kawaida wanapiga simu hadi saa 9 za usiku tunajadili ni vipi tunalipeleka jambo letu”

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SIMBA YAMFUTA KAZI KOCHA GOMES

 

Tupia Comments