Stori ya kifahamu leo March 24, 2018 ni kuhusu Tume ya vyuo vikuu Tanzania imesema haifanyi makusudi kuvifungia vyuo bali kinachofanyika ni kuvifungia vyuo ambavyo vimeshindwa kujiendesha pamoja na kutoa elimu bora.
Katibu mtendaji wa tume ya vyuo vikuu Tanzania Profesa Charles Kihampa akizungumza kwenye kongamano la baraza la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki linalofanyika jijini Nairobi nchini Kenya amesema wataendelea kuvijengea uwezo ikiwemo kuishauri serikali katika kutoa mikopo.