Ad
Ad

Mix

“Kila kitu kwenye maisha kimegusa Sanaa na Sanaa imegusa Maisha” – Vanessa

on

Mwimbaji wa Bongofleva Vanessa Mdee amefunguka kupitia XXL ya Clouds FM leo June 16, 2017 na kusema kuonekana kwake kwenye video akiwa anawabusu mwanaume ni sehemu tu ya kazi kama afanyavyo mpenzi wake Jux.

Vanessa ameyasema hayo wakati anaelezea namna alivyoonekana kwenye Red Carpet ya tuzo za Billboard na jinsi alivyopata deal la kuigiza Tamthiliya ya Shuga na kuelezea kuonekana kwake akimkiss mwanaume mwingine kwenye Tamthiliya hiyo.

>>>”…jamani si ni kazi? Halafu mimi ni muigizaji. Kwenye Shuga nimeigiza hiyo show ina mafunzo kama mtu akiangalia kwa makini atapata kitu kikubwa sana. Nawasihi wadogo zangu na Watanzania wakaiangalie watapata kitu.

“Halafu kwenye nyimbo kwani Jux akiwa na mademu wake huko kwenye ma-video wanashikana shikana inakuwaje sasa? Hamna kulipana sema kila kitu kwenye maisha kimegusa sanaa na sanaa imegusa maisha.” – Vanessa.

ON AIR: ‘Haikuwa rahisi, Jux aliniambia Mimi Mars anaweza’ Quick Rocka

VIDEO: Jux aeleza sababu za kwa nini Diamond hampost Instagram…

Soma na hizi

Tupia Comments