Michezo

Azam FC imetoa kipigo cha pili mfululizo kwa Simba ndani ya mwaka 2017

on

Siku 15 baada ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza dhidi ya Azam FC katika fainali ya Mapinduzi Cup 2017 January 13 visiwani Zanzibar na Simba kupoteza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Himid Mao, leo January 28 2017 timu hizo zilikutana tena katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Simba na Azam FC leo wamekutana katika uwanja wa Taifa Dar es salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, ikiwa huu ni mchezo wao wa 18 kwa Simba na Azam FC kukutana katika mechi za Ligi Kuu, Simba ikiwa imeifunga Azam FC mara 8, sare mara 5.

Leo January 28 nahodha wa Azam FC John Bocco anaipatia ushindi Azam FC wa goli 1-0, goli ambalo amelifunga dakika ya 71 kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Simba raia wa Ghana Daniel Agyei, ushindi huo wa Azam FC kwa Simba unakuwa wa 5 katika Ligi Kuu Tanzania bara toka waanze kukutana.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments