AyoTV

VIDEO: Sababu iliyofanya kocha Hans afute uamuzi wake wa kujiuzulu Yanga

on

Siku nne baada ya kocha wa Yanga muholanzi Hans van Pluijm atangaze kujiuzulu nafasi yake ya ukocha ndani ya Yanga kutokana na kuona kama anakosewa heshima ya nafasi yake kuhusishwa kutaka kupewa kocha wa Zesco United ya Zambia George Lwandamina, leo October 28 2016 amefuta maamuzi hayo.

“Nafikiri ni kutokana na majadiliano chanya tuliuofanya na mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, nafikiri yeye ndio kachangia kwa kiasi kikubwa mimi kubadili maamuzi, ukiachilia mbali mimi kukubali kubadili maamuzi kutokana na majadiliano yetu na waziri, mimi ni Kocha na nataka kufanya kazi”

“Baada ya kipindi kifupi kigumu kumalizika hivi vitu vipo katika soka, tulifanya majadiliano usiku wa jana na tumefanya majadiliano asubuhi ya leo nimeamua kurudi kazini kuanzia kesho asubuhi Jumamosi na jumapili nitakuwa kwenye benchi katika mchezo dhidi ya Mbao FC”

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments