Michezo

Bado siku 10 AFCON 2019, Kenya wanapata pigo

on

Ikiwa zimesalia siku 10 tuweze kushuhudia fainali za mataifa ya Afrika 2019 zianze nchini, timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars inawezeka akamkosa Brian Mandela.

Kenya wanaojiandaa na mchezo wao wa ufunguzi June 23 dhidi ya Algeria, wamepata pigo kufuatia beki wao Brian Mandela kuondolewa katika kikosi hicho kutokana na kuumia goti akiwa mazoezini.

Brian ambaye yupo Paris Ufaransa kambini na wenzake amepata pigo kufuatia kuumia kwa glti akiwa mazoezini na kocha wa Harambee Stars Sebastien Migne amemuondoa katika hesabu kwa kuaminika ameumia sana, Kenya wapo Kundi C na timu za Tanzania, Algeria na Senegal.

Soma na hizi

Tupia Comments