Michezo

Messi ameibuka mshindi wa FIFA 2019, Ronaldo hajatokea

on

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo lilihitimisha kilele cha utoaji wa tuzo za FIFA The Best 2019 kwa kutangaza wachezaji mbalimbali waliofanikiwa kushinda.

Tuzo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu ni tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kiume ambapo ilikuwa ikiwaniwa na Virgil van Dijk wa Liverpool, Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa FC Barcelona.

Ronaldo hakutokea katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika Italia na Lionel Messi kuibuka mshindi kwa mwaka 2019 na kuwashinda Ronaldo na Van Dijk, hii ndio mara ya kwanza kwa Messi kushinda tuzo hiyo toka mfumo mpya uanzishwe.

Jurgen Klopp wa Liverpool akiibuka kocha bora wa mwaka, Megan Rapinoe raia wa Marekani akiibuka mchezaji bora wa mwaka wa kike.

 

Soma na hizi

Tupia Comments