Maandamano ya kupinga Serikali huko nchini Bangladesh yamesababisha machafuko kati ya Polisi na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambapo baadhi ya Waandamanaji wanadai walitaka kufanya maandamano kwa amani lakini Jeshi la Polisi limeingilia na kutumia nguvu kubwa kuwadhibiti
Inaripotiwa Vijana wengi walioshiriki Maandamano wamefikishwa Hospitali wakiwa na majeraha ya risasi ambapo Serikali imelaumu Wapinzani wa Kisiasa kwa machafuko hayo yaliyotokana na malalamiko kuhusu mgawo wa nafasi za kazi Serikalini
Serikali ilizima Intaneti kwa siku kadhaa na kuanza kurejesha katika taasisi chache zikiwemo Benki, Kampuni za Teknolojia na Vyombo vya Habari ambapo amri ya kutotoka nje bado inatekelezwa na maelfu ya wanajeshi.
Muunganisho mdogo wa intaneti umerejeshwa Jumanne usiku, huku kipaumbele kikipewa makampuni kama vile benki, makampuni ya teknolojia na vyombo vya habari.
Ghasia hizo ni changamoto kubwa zaidi katika miaka mingi kwa Sheikh Hasina, 76, ambaye alipata muhula wake wa nne mfululizo kama waziri mkuu mwezi Januari, katika uchaguzi wenye utata uliosusiwa na vyama vikuu vya upinzani nchini humo.
Vikosi vya usalama vinashutumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi lakini serikali imewalaumu wapinzani wa kisiasa kwa machafuko hayo, ambayo yalizuka baada ya mgawo wa nafasi za kazi serikalini.