Kampuni ya Smile Communications Tanzania inatarajia kupokea dola za kimarekani milioni 120 kutoka kampuni ya Al-Nahla Group ambayo kwa sasa inamiliki asilimia 100 ya kampuni hiyo kupitia miongoni mwa kampuni zake iitwayo 966 Co. S.a.r.l ambapo hii ni baada ya uongozi wa kampuni za Al-Nahla Group na kampuni ya Smile Telecom Holding ambayo inafanya kazi kwenye nchi zikiwemo Tanzania, Nigeria, Uganda na DR Congo kukubaliana kujiimarisha kwa lengo ka kuongeza utoaji huduma nchini Tanzania.
“Uwekezaji huu kwetu ni jambo la furaha na matumaini yetu ni kwamba uwekezaji huu utakuwa chachu ya utoaji huduma zetu kwenye soko la mawasiliano na unaendana na dira na mkakati wetu. Uwekezaji wetu utachangia upatikanaji wa huduma za mawasiliano endelevu yaani 4G LTE kwa watu wote wanaoishi nchini Tanzania na utaleta manufaa makubwa ya kijamii kwa watumiaji” alisema Bw Ahmad Farroukh, Mkurugenzi Mtendaji wa Smile Group na Mwenyekiti wa bodi ya Tanzania.
Aliongeza kuwa “Uwekezaji huu utatengeneza fursa nyingi zaidi kwa Watanzania katika nyanja ya ushirikishwaji wa kidijitali huku akisisitiza kuwa kampuni ya Smile Communications imekuwa ikipanua shughuli zake, na kwa sasa huduma zake zinapatikana maeneo mengi nchini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita huku nakuongeza kuwa idadi ya wateja wake imekuwa pia na kusistitza kuwa baada ya kukamilisha mpango wa kimkakati wa kujiimarisha ambao ulitangazwa mnano febuari 2022, kampuni yake imeendelea kutoa huduma kama kawaida na kusema ufadhili mpya itasaidia kamuni ya Smile Telecoms Group kujiimarisha zaidi, kuongeza wigo na kutimiza malengo yake ya kibiashara.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Smile Communications nchini Tanzania Zuweina Farah, kampuni itatoa kipaumbele kuwezesha upatikanaji wa huduma zenye kasi zaidi na za kimataifa za mtandao na sauti “Tumewekeza katika uundaji upya na upanuzi wa mtandao wetu ili kuwapa wateja wetu huduma zilizoboreshwa za mtandao na kasi zaidi. Ukuaji wa wateja wa Smile katika kipindi cha miaka miwili iliyopita umekuwa mzuri sana, na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wetu” alisema Bi. Zuweina Farah.
Aliongeza kuwa kampuni yake inatarajia kupanua huduma zake nchi nzima huku akitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania, hususan Wizara ya TEHAMA, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuendelea kuungwa mkono juhudi za kampuni yake.
“Tumejizatiti kuendelea kutoa huduma bora za mawasiliano nchini Tanzania. Wateja wetu waendelea kutunga mkono na wategemee mengi mazuri kutoka kwetu,” alisema Farah.
Kampuni ya Al Nahla Group lilianzishwa na marehemu H.E. Hassan Abbas Sharbatly, ambaye hapo awali alianzisha Benki ya Riyad. Leo kampuni hiyo inamiliki hisa asilimia 9 ya Benki ya Riyad, iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Saudi.
Kampuni hiyo ya kifamilia inaangazia sekta za magari, mali isiyohamishika, biashara, biashara za baharini, nishati mbadala, mawasiliano ya simu na uwekezaji. Uwekezaji wake unalenga Falme za Kiarabu (Saudi Arabia), Ghuba, Misri na sekta chache za viwanda barani Afrika, pamoja na Smile Telecom Holding Group ikiwa ni mmoja wao.