Kikundi cha waasi wa M23 kinadaiwa kuwa kinaendelea kusonga mbele kuelekea maeneo ya kusini mwa jimbo la Kivu mara baada ya kutwaa jimbo la Goma, shirika la habari la AFP lilisema siku ya Jumatano.
Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na jeshi la DRC kuhusu uvamizi unaoendelea wa waasi wa M23.
Wakati huo huo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati uvamizi unaofanywa na kikundi hicho.
Hata hivyo, hali ya utulivu imeanza kurudi katika eneo la Goma lililopo Kivu Kaskazini, huku baadhi ya wakazi wakianza kurejea kwenye makazi yao.
“Hatuna hofu yoyote siku ya leo,” alisema Jean de Dieu mkazi wa Goma katika mahojiano yake kwa njia ya simu na AFP.
“Kuna njaa Goma. Inatubidi tufuate maji kutoka ziwani na hatuna dawa,” alisema mkazi mwingine aliyejitambulisha kama Kahi ndo Sifa
Licha ya shinikizo la kimataifa la kutatua mgogoro huo, Rais wa DRC Felix Tshisekedi aligoma kuhudhuria mazungumzo kati yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame, yaliyoandaliwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) siku ya Jumatano.