Wakati California ikiendelea kukabiliwa na Janga la moto Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Joe Biden ametangaza malipo ya Dola $770 kwa Kila mwathiriwa Sawa na 1,944,250 za Kitanzania kugharamia mahitaji muhimu kwa walioathiriwa na moto huo
Biden amesema hayo katika kikao fupi kilichofanyika Jana Januari 13, 2025 usiku na Makamu wa Rais Kamala Harris na maafisa wa dharura, ambapo Biden aliahidi kufidia 100% ya gharama za kukabiliana na maafa kwa miezi sita ijayo.
Pia alisisitiza usaidizi wa haraka kwa waathiriwa, ikiwa ni pamoja na malipo ya ya $770 kwa kila mkazi kwaajili ya mahitaji muhimu
Takribani msaada wa dola milioni 5.1 tayari zimesambazwa, na takribani wakazi 33,000 wamejiandikisha kwaajili ya kupata msaada kupitia shirika la serikali ya Marekani ambalo hushughulikia maafa yaliyotangazwa na Rais (FEMA)
Serikali ya Biden pia inashughulikia gharama zote za kuzima moto kwa siku 180, ambapo jumla ya wanajeshi 1,800 wa Walinzi wa Kitaifa wametumwa na teknolojia ya infrared ikitolewa kusaidia juhudi dhidi ya moto unaowaka katika Palisades ya Pasifiki, Eaton Canyon, na maeneo mengine.