Idadi kubwa ya wabunge wanamkata Biden kutoa afueni ili kuzuia mtandao wa TikTok kufungwa nchini Marekani ifikapo Jumapili, na kuonya kuwa mamilioni ya wabunifu na biashara zinaweza kuathiriwa.
“Tunaomba kuwepo njia ya kujaribu kusuluhisha suala hili kwa busara ili TikTok isijikute katika hali ngumu,” Seneta Mdemocrat Ed Markey alisema Alhamisi.
“Tusubiri, tujaribu kurudi nyuma, tuchukuwe muda zaidi, tujaribu kulifikiria hili.”
Kiongozi wa Wademocrats katika Baraza la Seneti Chuck Schumer alizungumza na Biden na kumtaka kuongeza muda wa mwisho kwa siku 90 kwa kampuni miliki ya China ByteDance ili kuuza mali za TikTok kwa mmiliki Mmarekani na kuzuia marufuku ya mtandao huo unaotumiwa na Wamarekani milioni 170, Schumer alisema.