Top Stories

Wabunge wataka Benki ya Dunia kufuta madeni

on

Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wametoa wito kwa shirika la Fedha la kimataifa (IMF) na Benki ya dunia kufuta madeni kwa nchi masikini.

Zaidi ya wabunge 300 kutoka nchi ishirini wametoa wito huo leo kwa kutaka kufutwa madeni kwa nchi masikini zinazokabiliwa na athari za kiuchumi zinazotokana na janga la Corona.

Seneta wa Marekani Bernie Sanders, ambaye ni mmoja wa waasisi wa mpango huo pamoja na mbunge kutoka Chama cha Democratic Ilhan Omar, amesema nchi masikini zinatakiwa kulinda raia wao badala ya kulipa mzigo mkubwa wa madeni kutoka kwa taasisi kuu za kifedha za kimataifa.

Nchi mbalimbali zinabaini kwamba ulipaji wa madeni kwa nchi masikini zaidi unapaswa kufutwa kabisa badala ya kusitishwa tu, kama zilivyoamua nchi zilizoendelea kiviwanda na zinazoinukia kwa kasi kiuchumi G20 mnamo mwezi wa Aprili mwaka huu.

LIGI KUU KUREJEA, “MASHABIKI HAWAIINGII UWANJANI”, WAMILIKI VIBANDA UMIZA WAJIPANGA

Soma na hizi

Tupia Comments