Michezo

Wachezaji Bayern Munich wakatwa mishahara

on

Club ya FC Bayern Munich ya Ujerumani imewakata mishahara wachezaji wake watano (Serge Gnabry, Joshua Kimmich, Jamal Musiala, Eric Maxim Choupo-Moting na Michael Cuisance) kama adhabu kwa kosa la kutochoma chanjo ya COVID-19 wakati huu ambao inadaiwa visa vya CORONA Ujerumani vinaongezeka.

Bayern Munich wiki iliyopita iliwataarifu wachezaji wake kuwa haitowalipa wote ambao watakosekana katika shughuli za club kutokana na kukosa chanjo ya COVID-19.

Mambo yamekuwa makubwa zaidi wiki iliyopita baada ya wachezaji wawili wa Bayern Niklas Sule na Josip Stanisic kukutwa na maambukizi ya virusi vya CORONA huku Serge Gnabry, Joshua Kimmich, Jamal Musiala, Eric Maxim Choupo-Moting na Michael Cuisance watakiwa kukaa karantini kutokana na kukutana na wachezaji hao.

WAVAMIZI WAUA TWIGA, SWALA “WACHOMA SHAMBA, MALI ZAIDI MILIONI 60 ZATEKETEA”

Soma na hizi

Tupia Comments