China imepiga marufuku Wachezaji wa mpira kujichora tattoo kwenye miili yao na kuamuru wote walio na tattoo waziondoe au kuzifunika ili kuwa “mfano mzuri kwa jamii,”, limeeleza agizo lililotolewa na Utawala Mkuu wa Michezo wa China (GAS).
Maagizo hayo yenye mada “Mapendekezo ya kuimarisha usimamizi wa Wachezaji wa soka” yanaweka masharti ya kinidhamu kwa Wachezaji wa timu ya taifa “Wanariadha wa Timu ya Taifa na Timu ya Taifa ya U23 wamepigwa marufuku kabisa kujichora tattoo mpya”.
“Wale ambao wana tattoos wanashauriwa kuondoa tattoos wao wenyewe ama ni lazima wazifunike wakati wa mafunzo na mashindano, Timu za kitaifa katika viwango vya chini ya miaka 20 haziruhusiwi kuajiri Wanariadha wapya wenye michoro hiyo mwilini”
Hii sio mara ya kwanza kwa China kutoa onyo kuhusu tattoos kwani mwaka wa 2018 Mdhibiti wa vyombo vya habari nchini China alitoa amri akisema Televisheni ya China haipaswi kuwapa nafasi Waigizaji wenye michoro ya tattoo ambapo agizo hilo lilifanya picha zilizo na tattoos kuzibwa kwa ‘ukungu’ kabla ya kuonyeshwa kwenye TV.