Michezo

Wachezaji wa Raja Casablanca watakiwa karantini

on

Wizara ya afya nchini Morocco imeitaka club ya Raja Casablanca kujiweka karantini sababu ya wachezaji wake 9 kupimwa na kukutwa na Corona baada ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Zamalek ya Misri.

Kwenye mchezo huo Raja Casablanca walipoteza kwa goli 1-0 na watatakiwa kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Zamalek Jumamosi hii nchini Misri.

Hata hivyo muda mfupi uliopita CAF wametangaza kuwa mchezo wa marudiano uliyokuwa uchezwe weekend hii umeahirishwa kutokana na Raja Casablanca kutakiwa kuingia karantini.

Soma na hizi

Tupia Comments