Wakati Serikali ikiendelea na kutoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa maporomoko Wilayani Hanang Mkoani Manyara baadhi ya wadau mbalimbali mkoani Morogoro wameguswa na janga hilo na kuanza kuchangia Msaada kwa waathirika.
Viridium Tanzania LTD Ni mmoja kati ya wadau walioguswa na kutoa tani kumi za nishati ya mkaa mbadala (MKAA MWEUPE)ambao umetengenezwa kwa kutumia majani ambao hauna athari kimazingira.
Akizungunza wakati wa kukabidhi msaada kwa Mkuu wà Mkoa Morogoro, Meneja Masoko wa kampuni hiyo ya Viridium Tz Limited Bwana Aristotle Nikitas anasema Rais Samia anasisitiza matumizi ya nishati mbadala ili kuacha kuharibu misitu kwa kutumia mkaa wa kawaida na kuni hivyo wameona wamuunge mkono kwa kuonesha mfano kwa jamii matumizi ya Mkaa huo mbadala.
Anasema wadau wengi wamepeleka msaada wa chakula na nguo hivyo ,majiko na mkaa itasaidia waathirika hao ambao katika matumizi ya nyumbani.
Naye Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima akipokea msaada huo ameipongeza kampuni hiyo kwa kujitoa kuonesha mfano wa utunzaji Mazingira huku akibainisha kua Serikali ya mkoa pia inafanya utaratibu wa kupeleka misaada katika Wilaya hiyo ili kuwasadia Waathirika hao.
RC Malima amesema msaada huo umeenda sambamba na maono ya Rais Samia ya kwenda kushiriki mkutano Dubai wa Utunzaji mazingira hivyo mkoa utahakikisha unaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine katika utunzaji mazingira.
Aidha RC Malima amesema licha ya Mkoa Morogoro kukumbwa na mafuriko katika baadhi ya maeneo Wilayani kilosa tayari misaada mbalimbali imeanza kupelekwa kwa waathirika wilayani humo ili kuwasadia kama maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa waathirika hao kupatiwa mahitaji muhimu ikiwemo chakula,mavazi na matibabu.