Wadau wa elimu wakiwemo Camfed wametakiwa kuendelea kushirikiana na wadau wengine na serikali katika programu zake zenye lengo la kusaidia watoto hasa wakike kwenye suala la elimu kwa kuongeza kasi na uwekezaji wa sera mpya iliyoboreshwa.
Hayo yamesemwa na Ernest Hinju Mkurugenzi msaidizi elimu ya watu wazima na elimu maalumu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Camfed Tanzania na hafla ya kushirikisha wadau uliofanyika mkoani Morogoro.
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Camfed Tanzania Bi Nasikiwa Duke wameeleza kuwa shirika lao limewasaidia Wanafunzi 604 kuhitimu vyuo 2024 katika programu yao ambopo zaidi ya wahitimu 500 wamepatiwa hajira kama zao la Camfed lakini pia kiujumla asilimia 54 ya wafanyakazi ya camferd ni mazao yao.
Sambamba na hayo ameishukuru serikali na wadau wengine Kwa ushirikiano wao wanao onesha Kwa Camfed katika kuimarisha na kuendeleza programu ya kusaidia wanawake kwenye swala la elimu na kutoa mitaji
Katika mkutano huo mwalimu Ephraim Simbeye Mkurugenzi udhibiti ubora wa mashule Kutoka wizara ya elimu sayansi na Teknologia, amesema wao kama wizara wanaendelea kuimiza kaulimbiu ya utekelezaji Kwa mtaala ulioboreshwa pamoja na utekelezaji elimu ya amani asaasa shule za secondary ivyo waendelee kusimamia utaala huo ambao kimsingi ni maelekezo ya wizara.
Hata hivyo Froriana kitinye ni mnufaika Kwa upande wa elimu ngazi ya Chuo kikuu amesema amesomeshwa kuanzia kidato Cha kwanza mpaka chuo kwani kabla ajaanza kufadhiriwa na shirika maisha yalikuwa magumu huku Saida Rashidi muya upande wa biashara nae amesema kupitia comfed amejikwamua kimaisha baada ya kufadhiriwa mtaji.