Wadau wa maonesho ya mitindo nchini wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya matukio hayo ili kuimarisha ufanisi na weledi ndani ya tasnia hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi wa msimu wa nne wa Safari Fashion Weekend, unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, muandaaji wa jukwaa hilo, Bi. Lily Massa, amesema dhamira ya mwaka huu ni kuiunganisha mitindo na asili kwa kuonyesha mavazi na vyakula vya kiasili kutoka kwa makabila mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Tunataka kuleta mtazamo mpya kwa kuhusisha asili na mitindo, tukionyesha urithi wa tamaduni zetu kupitia mavazi na chakula cha kiasili,” alisema Lily Massa.
Kwa upande wao, wadau waliokuwepo kwenye uzinduzi huo wamesisitiza umuhimu wa kushiriki katika majukwaa kama haya ili kuendeleza tasnia ya mitindo na kuleta fursa kwa vijana.