Wadau wa Mazingira na utalii wametakiwa kuwa mabalozi kwa kutunza vivutio vya asili Ili jamii inayowazunguka iige
mfano kutoka kwao.
Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili iliofanyika katika ukumbi wa hotel ya Sunset Iringa mjini mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Joachim Nyingo ambae alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema kampeni hii ya kutunza na kuuhifadhi mlima udzungwa ni jukumu la Kila mtu.
Nyingo amesema wataalamu wajitahidi kutoa elimu ya uhifadhi wa Mazingira kwa wananchi kwa maslahi mapama ya Taifa kwa ujumla lli kuendelea kuikuza hifadhi ya udzungwa kwa Miaka 20 ijayo .
Aidha Meneja mradi wa mradi wa mpango mkakati wa kuhifadhi ya mlima Udzungwa UDZUNGWA LANDSCAPE STRATEGY Arafat Mtui amesema lengo kuu ni kuboresha shuhuli za uhifadhi katika hifadhi tatu ikiwemo hifadhi ya Taifa ya udzungwa, pia kuboresha uhusiano mzuri kati ya wananchi waliozunguka hifadhi hiyo na mamlaka za hifadhi
Mtui aliongeza na kusema kwenye hifadhi ya mlima Udzungwa Kuna nishati mbadala zinazopatikana nishati ambazo zinatokana na takataka mbalimbali ambazo zinatengeneza mkaa mbadala.
Kwa upande wake Afisa wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na utalii Bi. Rose Mdendemi amesema mkakati wa serikali ni kupunguza migongano baina ya wanyamapori na binadamu lengo kuu ni kutunza Mazingira.
Bi Rose amesema shoroba nyingi zinakuepo kwenye hifadhi nyingi lakini serikali inaendelea kushirikiana na jamii Ili shoroba hizo zinaondolewa Ili wanyama wawe huru na binadamu wawe Wana sehemu yao kusiwe na muingiliano.
Warsha hii imeandaliwa na wadau pamoja na mashirika mbalimbali kama STEP, MAZINGIRA na REFOREST AFRICA lengo kuu likiwa ni kutunza Mazingira hasa yanayozunguka hifadhi za Taifa ikiwemo hifadhi ya mlima ya udzungwa.