Kampuni ya Silverlands inayoshughulika na uzalishaji wa vifaranga na chakula cha kuku imesema inaanzisha mpango mahususi utakaoishirikiana na Programu ya BBT Mifugo kuunga mkono jitihada za Mheshimwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwawezesha vijana na akinamama katika sekta ya ufugaji ili kukuza uchumi jumuishi na kupunguza mikopo kausha damu kwenye jamii.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizinduzia mtambo wa kuangua Vifaranga vya kuku katika hafla iliyofanyika Mkoani Arusha Agosti 2, 2023.
“Mipango yetu katika tasnia ya kuku kwa sasa, ni kuibadilisha tasnia kutoka kwenye ufugaji wa kimazoea kwenda kwenye ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji. Nawataarifu Watanzania wote kwamba sasa Silverlands wako na BBT kwa upande wa ufugaji kuku. Kwa msingi huo nawakaribisha na wawekezaji wengine wanofanya kazi hii ya kuku na wao kuungana na serikali” Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.
Waziri Ulega ameeleza kwamba BBT inafanya vizuri kwenye upande wa mazao, ufugaji wa ng’ombe na Samaki, na hivyo anawakaribisha wawekezaji waingie pia kwenye ufugaji wa kuku ambao unapendwa zaidi na vijana na kimanana wengi.