Baada ya kuibuka sakata la Tanga Cement na Twiga Cement, hoja mbalimbali zimeendelea kuibuka ikiwemo juu ya pande ambazo hazijawahi kusikika.
Miongoni kwa wadau wanaotajwa kwamba hawajawahi kusikika ni zile pande ambazo zilikata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania ya Ushindani wa Haki.
Baadhi ya wakataji rufaa hao waliwahi kuiburuta Serikali mahakamani ambapo walalamikaji ndio pekee waliokuwa wakitoa hoja zao.
“Sio Heidelberg / Twiga wala Tanga, rufaa nyingi tayari zimetupiliwa mbali na Mahakama kutokana na kutokuwa za kweli,”
“Pia ikumbukwe kuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji, alionesha uthibitisho kwamba Chalinze Cement inaonekana ilidanganya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),”.
“Inawezekana makundi hayo ya siri yanaweza kueleza uongo kwa FCT na mahakamani pia walianzisha mashambulizi mengine kupitia vyombo vya habari. Kampeni yao ni ya makusudi na ya kueneza habari potofu,”. Amesema mmoja wa wadau wa Maendeleo.