Top Stories

“Wafanyabiashara tangazeni utalii wa Tanzania” Naibu Waziri

on

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa wito kwa wafanyabiashara na wamiliki wa makampuni nchini kuunga mkono jitihada inazozifanya za kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini kupitia biashara zao.

Wito huo umetolewa Jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja kwenye maonesho ya biashara, uwekezaji na utalii yanayojumuisha wadau mbalimbali.

Masanja amesema kuwa wafanyabiashara ni wadau wakubwa wa sekta hivyo hivyo wana nafasi kubwa wa kuitangaza ili kusaidia kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini.

“Nawaomba sana nyinyi wafanyabiashara kupitia makampuni yenu mtangaze utalii wa Tanzania na vivutio vyake kwakuwa nyinyi ni wadau wakubwa wa sekta hii,” Masanja.

Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema kuwa wafanyabiashara kama watakuwa na mahusiano mazuri wataweza kuinua uchumi wa nchi ikiwemo kuutangaza utalii.

MEI MOSI: “TULIKUJA NA MATARAJIO YAKUONGEZWA, HATA KWA PUNGUZO TUNASHUKURU”

Soma na hizi

Tupia Comments