Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalage amewataka wenye maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na karatasi iliyoandikwa na daktari.
Dkt Seif aliyasema hayo leo mjini Tanga wakati akifungua kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.
Alisema jambo hilo ni la msingi na Serikali wameweka sheria kali mtu akimakatwa anachukuliwa hatua lakini sasa wanazungumza wanaofanya kwa njia za siri ambao hawajagundulika wanasababisha tatizo linakuwa kubwa.
“Katika hili napenda kusisitiza hili kwa wenye maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na karatasi iliyoandikwa daktari”Alisema
Alisema waanajua zipo dawa muhimu zilizowekwa kwenye maduka lakini dawa za antibayotiki wananchi wasitumie tu kwa sababu wanapotumia dawa bila kupata ushauri kwa daktari dawa za aina gani kwa sababu kufanya hivyo wanatengeneza mwili wao kuwa na usugu vimelea vinavyokupata kuweza ku kutibiwa na zile dawa ambazo ni sahihi kwa sababu umeshatengeneza usugu wa kuweza kutrumia tu dawa,
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Said Aboud
ametoa wito kwa wananchi kuto kwenda duka la dawa kununua dawa bila cheti cha daktari kwani kumekuwa na mazoezi wananchi kwenda kujinunulia dawa bila kujua kama kweli wanahitaji kutumia hizo au la.
Alisema pia vilevile wanapoandikiwa dawa za daktari wahakikishe wanatumia dozi kamili na wanatumia kwa mujibu ilivyoandikwa na Daktari.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Dkt Naima Yusuf amesisitiza wananchi kuacha kutumia dawa bila kujua wanaumwa na nini kwani kufanya hivyo zinaweza kuwasababishia madhara mbalimbali.
Alisema katika utafiti huo walichofanya walichukua sampuli kutoka kwa mama na mtoto aliyezaliwa na kama amezaliwa kwa njia ya kawaida au upasuaji na vifaa vilivyotumika.
“Tupo hapa kwa ajili ya kusisitiza wananchi wasitumie dawa bila kujua wanaumwa na nini kwani kuna tabia unaumwa kidogo unakwenda duka la dawa unachukua dawa mwishowe zile dawa zinaacha kufanya kazi”Alisema