Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya Kampuni ya kimataifa ya ABInBEV, imekutana jijini DSM na wasambazaji wa bidhaa zake kutoka nchini pote kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuboresha zaidi usambazaji.
Sambamba na kuwashukuru ambapo wasambazaji bora wawili wamejipatia zawadi ya magari ya kubeba mizigo kwa ajili ya kurahisisha usambazaji wa bidhaa kwa wateja na wasambazaji wengi wamejipatia vyeti na vikombe vya kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.
Mbali na wasambazaji wafanyakazi wa kitengo cha mauzo wa TBL, nao wamezawadiwa tuzo kutokana na kazi nzuri wanayoendelea kufanya katika kufanikisha malengo ya kampuni ya kuendelea kuwa kampuni bora ya bia inayoongoza nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Philip Redman (kulia) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari Happyness Joseph (Katikati) kutoka Fresa Investment baada ya kuibuka msambazaji bora mwaka 2019 na kujishindia lori la usambazaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Philip Redman (kushoto) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari Richard Justine kutoka Mbeya baada ya kuibuka msambazaji bora namba mwaka 2019 na kujishindia lori la usambazaji.
Wasambazaji katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TBL,Philip Redman (katikati) baada ya kukabidhiwa zawadi na tuzo.
Baadhi ya wafanyakazi wa matzo wakifurahi na Mkurugenzi Mkuu baada ya kushinda tuzu
Wafanyakazi wa kitengo cha mauzo wakionyesha tuzo zao katika hafla hiyo