Katika juhudi za kuimarisha sekta ya ufugaji na kuboresha ustawi wa jamii, Kampuni ya Asas imetekeleza ahadi yake iliyotolewa wakati wa Sherehe za Kizimkazi Festival kwa kuandaa ziara ya wafugaji kutoka Kizimkazi kwenda kwenye mashamba yake yaliyopo Iringa.
Itakumbukwa Mnamo Agosti 8, 2024 kampuni ya Asas iliahidi kuwapa wafugaji wa Kizimkazi fursa ya kujifunza mbinu za kisasa za Ufugaji katika mashamba yake.
Sasa hatimae ahadi hiyo imetekelezwa na tunaye Mwakilishi wa Kampuni ya unywaji na uuzaji wa maziwa ya Asas akieleza namna wafugaji wa Kimzikazi walivyopata Elimu na Fursa juu ya ufugaji.
“Kama utakumbuka kwenye Sherehe za Kizimkazi Festival tuliahidi kuwaleta wafugaji wa Kizimkazi katika Mashamba yetu na hatimae tumetekeleza, na ziara hii kwa wafugaji hawa imetufungulia macho, na maarifa mapya ambayo yakitumika vizuri yatasadia kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha yetu”- Msemaji wa kampuni ya Asas
“Katika ziara hii, wafugaji wapatao 50 walipata nafasi ya kushuhudia mifumo ya kisasa ya malisho, mbinu za matibabu ya mifugo, na usindikaji wa maziwa. Aidha, walipata elimu juu ya jinsi ya kuboresha uzalishaji na kudumisha afya ya mifugo yao kwa njia endelevu”- Msemaji wa kampuni ya Asas
“Kwa miaka mingi, Asas imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono maendeleo ya kilimo na ufugaji, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa uwajibikaji wa kijamii. Utekelezaji wa ahadi hii unadhihirisha dhamira ya dhati ya kusaidia wafugaji wadogo ili kuongeza kipato na kuboresha maisha yao”- Msemaji wa kampuni ya Asas
“Ziara hii ni mwanzo wa ushirikiano endelevu na inatarajiwa kuleta mabadiliko chanya kwa wafugaji wa Kizimkazi na maeneo mengine nchini Tanzania”- Msemaji wa kampuni ya Asas
Asas imeonyesha kuwa sekta binafsi inaweza kuchangia maendeleo ya kijamii kwa vitendo kupitia uwekezaji katika elimu na mafunzo kwa jamii za wafugaji.
Kampuni hiyo imejidhatiti kuendelea kushirikiana na wafugaji wa maeneo mbalimbali ili kuboresha sekta ya ufugaji nchini.