Jeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo nchini (STPU) kimewahakikishia usalama wa mifugo yao wafugaji waliohama kwa hiari kutoka mamlaka hifadhi ya ngorongoro kuunga juhudi za uhifadhi nchini huku kikibainisha kuwa tayari kimeshapata majina ya watuhumiwa wanao jihusisha na wizi wa mifugo hapa nchini huku kikitoa onyo kwa watu wanaojihusisha na tabia hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Polisi kikosi cha kupambana na wizi wa mifugo nchini ACP Simon Pasua wakati wa kuwaaga wananchi waliohama kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kupisha shughuli za uhifadhi ambapo amesema sema Jamii hiyo yakifugaji inapaswa kutembea kifua mbele kwa sababu kikosi hicho kitahahakikisha mifugo yao inakuwa salama.
Ameongeza kuwa tayari Jeshi hilo limeweka utaratibu mzuri na Polisi kata ambao wamesha unda vikundi vya ulinzi wa mifugo hiyo, ambapo kikosi hicho kimepokea majina ya baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo.
Sambamba na hilo Kamanda Pasua amewaomba wafugaji kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi hususani kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo kwa kutoa taarifa za baadhi ya watu wananojihusisha na wizi wa mifugo ili Jeshi hilo liwachukulie hatua za kisheria.